Loading ...

0
Fursa 101 Africa Academy . 13th Jun, 2021

Je kuna Uhitaji wa kile Unachouza?

Kama unataka matokeo kwenye biashara na uwekezaji hakikisha unazingatia “M” sita.Usitegemee kwamba mwekezaji atakukubalia na kuwekeza kwako kama hutagusa maeneo sita ambayo mimi hupenda kuita “M”sita. Ngoja niende moja kwa moja kwenye “M” sita …


1. MASOKO
Unapokuwa kwenye biashara lazima ujue ni nani mteja wako. Lazima uchague soko lako. Wateja wako ni watu wa aina gani? Soko lako ni taasisi? Soko lako ni mtaani kwako? Mtandaoni? Nchi nzima? Soko lako ni watu wenye tabia gani? Wana kipato gani? Wana hela?
Kuna watu ambao wanauza bidhaa ambazo masoko yao hayawahitaji. Mtu anahangaika kutangaza kitu kwa watu wasiomhitaji.
Mimi huwa nafananisha soko kama mpenzi wako. Yaani lazima ujue mpenzi wako unayemtafuta ni wa aina gani? Anapenda nini? Anapenda ngono, anapenda hela, anapenda kuvaa, anapenda movie, anapenda kusoma, anapenda nini? Hili litakusaidia kujua kama unaweza kumridhisha ama la. Usiingie kwenye mahusiano ambayo huwezi kutimiza mahitaji , utaishia kupoteza ka mtaji kako kote na kuishia kusema “wanaume wote ni MBWA.” au “wanawake wote ni KUNGURU” kumbe kosa ni lako mwenyewe.

Kama soko halikutaki usilazimishe mapenzi. Utapoteza mtaji wako wote kwa kulazimishwa usipopendwa(yaani soko).
Anza kujiuliza huyo mpenzi wako anayeitwa soko anapenda nini? Je ana kitu unachohitaji?
Unaweza kuja na bidhaa nzuri au huduma ya kibabe au wazo kubwa la kimapinduzi lakini mwenye maamuzi ni soko. Soko ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho.

Lazima uhakikishe mambo mawili kwenye soko, JE KUNA UHITAJI? Kama watu hawatumii pesa zao kwenye hilo soko usipoteze muda wako hapo. Hakikisha kuwa kuna uhitaji na watu wanatumia hela kupata mahitaji hayo.
Jambo la pili , JE UNA NAFASI KWENYE HILO SOKO? Usipende kung’ang’ania kutoa mapenzi sehemu usipopendwa, jiulize kwanza nafasi yangu ipo? Wewe unaona kabisa kuna watu wanauza unachouza , yaani bidhaa zinafanana na zina ubora na mwonekano wa kufanana kwanini soko likuchague wewe na siyo mwingine. Je una nafasi kwenye soko? Una kitu gani spesho? Una nini Zaidi wewe mpaka soko likupendelee wewe? Una uzuri gani wewe? Una utofauti gani wewe? Jiulize jiulize…kabla hujaingia kwenye hilo soko.

Ukifanya kosa kwa kuingia kwenye soko bila kujibu maswali hayo basi fahamu kuwa biashara yako lazima lazima iangukie pua. Jipange kufunga vilago vyako na kupewa talaka tatu. Huna kitu cha tofauti unatafuta nini kwenye soko wakati huna utofauti na Mwajuma?
Kitu kingine lazima ujue undani wa hilo soko, mazingira ya hilo soko, nani ni suppliers, nani ni msambazaji, nani ni msafirishaji, utafikishaje ujumbe, utafikishaje bidhaa …hujui haya yote unategemea nini?






Shopping Cart

Loading...