Loading ...

0
Fursa 101 Africa Academy . 13th Jun, 2021

Jitathmini - Unapiga Hatua au Unatwanga Maji kwenye Kinu?

“M” ya tano ni MAENDELEO kitalaamu MILESTONES
UNASOGEA MBELE AU UNATWANGA MAJI KWENYE KINU?
MAENDELEO katika kila hatua.
Hapa ni pale unapopima maendeleo ya kile unachofanya. Huwezi kuwa kila siku ni kazi, asubuhi kazi, mchana kazi, usiku kazi …miezi inakatika, mwaka lakini hakuna hatua uliyopiga. Hukui wala huongezeki. Kulikoni? Lazima ifike wakati ujipime umefikia hatua gani? Umekua kiasi gani?
Asili ya Biashara ni kama kiumbe hai. Inatungwa, inazaliwa, inakua, inafikia makamo, inazeeka na kisha inakufa. Hivi ndivyo mifumo yote ya maisha inavyokwenda. Kuanzia kwetu sisi binadamu, kabla hujazaliwa mimba inatungwa, anazaliwa mtoto, anakua, anafikia makamo, anazeeka na kisha anakufa.
Biashara nayo ipo hivyo. Inaanza na utungwaji wa mimba ya biashara ambayo ni mawazo ya biashara. Baada ya hapo biashara inaanza ni sawa na mtoto anayezaliwa, biashara inaanza kukua na kukua kupitia mauzo, wafanyakazi, miradi, majengo, vitengo, tunasikia Dada Hilda amefungua branch Mwanza, oh kwasasa amefungua branch nyingine Nigeria, biashara inakua mpaka inazeeka na mwisho inakufa.
Sasa kama ilivyo kwenye asili, siyo mimba zote zinazotungwa zinazaliwa, nyingine zinaharibika kabla ya kufikia kuzaliwa. Kuna watu wanakujaga na mawazo mazuri ya biashara yanakufa hata kabla biashara haijaanza, wengi wapo humu. Na kuna watu wanaanzisha biashara kama kama watoto wadogo wanaozaliwa, wengi hawafiki utu uzima, wanakufa kabla. Na wachache wanafika utu uzima na kufa. Biashara zipo hivyo.
Biashara nyingi huwa zinashindwa kabla hata ya kuanza, nyingi zinaishia kwenye mawazo pekee. Kwa zile ambazo zinaanza, nyingi huwa zinakufa kwenye uchanga, hazikui kufikia ukomavu.
Ingawa wapo wajasiriamali wajanja, ili kuondokana na hali hiyo ya biashara kufika ukingoni na kufa, wafanyabiashara hao ambao biashara zao hazifi, wamekuwa wanakuja na bidhaa mpya au huduma mpya kila mara ambapo bidhaa au huduma ya zamani imefikia kilele chake cha mauzo. Hawasubiri mpaka mauzo yaanze kupungua na biashara kufa. Badala yake wanakuja na bidhaa au huduma mpya inayowafanya waendelee kuwa sokoni.
Ishu yangu kubwa leo ni wafanyabiashara wale ambao wapo busy sana lakini hatuoni kama wanakua wala kusogea mbele. Haieleweki kama biashara imekufa au inapumua. Utawaona wanakimbia kama vichaaa lakini hakuna matokeo yanayoonekana. Why? Ukiwa mfanyabiashara lazima uhakikishe unapima maendeleo yako ujue kama unapiga hatua au ndiyo unarudi nyuma au umekufa. Tangu uanze biashara umeuza kiasi gani? Una wateja wangapi wanaorudia kununua kutoka kwako? Wangapi?
Tangu uje na biashara hiyo umepiga hatua gani?
Hata wawekezaji kabla hajawekeza chochote kwako lazima akuulize hili swali, WHAT IS YOUR MILESTONES? Hapa anakuuliza tangu uanze biashara yako umepiga hatua gani? Umeuza kiasi gani? Una wateja wangapi wanaorudia kununua kwako? Umewekeza kiasi gani?
Kuna mtu eti ananipigia simu, Tengananamba nina wazo zuri la mobile app natafuta wawekezaji. Ukitaka kupata hela kutoka kwa mwekezaji lazima uonyeshe umepiga hatua gani tangu uanze biashara. Hakuna mtu anayetaka kuwekeza kwa mtu asiyeeleweka kama yupo hai au amekufa.
Nilichogundua ni kwamba wajasiriamali wengi wanaishi matumaini hewa. Hakuna hatua unayopiga kibiashara lakini unaenda tu ukiwa na matumaini kuwa labda mambo yatabadilika. Lazima ionekane umepiga hatua kiasi gani? Chochote unachofanya lazima upime matokeo yake, umefikia wapi?
Wewe kila siku ni biashara tu , upo busy vibaya mno. Huna hata muda lakini hakuna matokeo yanayoonekana hata kwako mwenyewe? Unafanya nini sasa?
Kaa chini jitathmini tangu uanze biashara umefanya nini? Umepiga hatua gani? Nini kimeongezeka. Kilichowafanya wengi kufa mapema ni kushindwa kukabili uhalisia ambao haukuwa mzuri kwao. Ni bora ujue moja kuwa sijapiga hatua ujue nini cha kufanya na hata ikibidi ubadili mwelekeo. Wengi wetu tunatumia mbinu ya mbuni kufukia kichwa chake kwenye mchanga ili asiione hatari, kwa kutokujua kwamba kuchagua kutokuiangalia hatari hakuifanyi iondoke.
Mbinu hii inamsaidia mtu asikabiliane na ukweli mchungu, lakini haiwezi kufanya kazi kwa muda mrefu, kadiri muda unavyokwenda na mambo kutokuwa kama mtu anavyotegemea, anakata tamaa na kufa au kuanguka. Jitathmini ujue unasogea mbele au unatwanga maji kwenye kinu.
Angalia biashara yako. Kama husogei mbele labda upo kwenye soko la ovyo yaani wrong market au mtindo wako wa biashara ni wa ovyo yaani hujui business model yako. Hata ufanye kazi kwa bidi masaa 24 kwa siku utabaki masikini bila chochote bila matokeo milele na milele amina.
Ili upige hatua, Kila wakati angalia ni hatua ipi ya tofauti unaweza kufanya kwenye kila kipande na biashara yako ikapiga hatua mpya.
Kwa upande wa wateja, angalia wapi unaweza kupata wateja wapya kwa bidhaa uliyonayo sasa, au kutengeneza bidhaa mpya kwa wateja ulionao sasa.
Kwa upande wa mahitaji, angalia ni mahitaji gani mapya ambayo wateja wako wanayo na unaweza kuyatimiza.
Kwa upande wa nafasi yako kwenye soko, angalia ni kwa namna gani unaweza kujitofautisha zaidi na washindani wako na wateja wakakufikiria wewe tu.
Na kwa upande wa ubobezi, angalia maeneo mapya unayoweza kubobea na ukawahudumia zaidi wateja ulionao au wateja wapya.
Kila wakati biashara yako inapaswa kutengeneza wateja wapya , kuongeza mauzo na kuwafanya wateja waliopo waendelee kununua na kununua. Kama biashara haitengenezi wateja wapya, na wale waliopo hawaendelei kununua, unafanya nini sasa hapo kama siyo kucheza kwaito.



Shopping Cart

Loading...