ü Mtatuzi wa matatizo. Wauzaji mashuhri ni wale wenye uwezo
wa kutatua matatizo. Lazima uwe na
mtazamo wa kutatua matatizo kwa kutoa suluhisho kwa wateja wako. Mfano kama
unafanya biashara ya magari lazima uwe na matazamo wa kutatua tatizo la usafiri
na usafirishaji. Kama unafanya biashara ya simu lazima uelewe kwamba upo ili
kutatua tatizo la mawasliano.
Kwa
hiyo kabla hujaingia kwenye sekta hii lazima uwe na mtazamo wa kutatua
tatizo.Kwanza lazima ulitambue na kulielewa vizuri tatizo kabla ya kujaribu
kulitatua. Hii itakusaidia kuwa mbunifu mzuri katika kuboresha huduma au bidhaa
yako ili kutatua tatizo husika ipasavyo. Na hii itakuwa ni dhumuni kuu
linalokusukuma.
ü Uwezo wa kupanua wigo zaidi ya ulipoanzia. Je
bidhaa au huduma unayouza unaweza
kuibadilisha ikakidhi kusudi au uhitaji mwingne ili kupanua wigo?
Je
bidhaa au huduma yako unaweza kubadili kukidhi uhitaji wa watu wengne zaidi wa
wale wa mwanzo? Mfano mwanzilishi wa Facebook bwana Mark Zuckerberg , wakati
anaanzisha Facebook ilikua kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa chuo alipokua
anasoma waweze kuwasiliana, lakin aligundua kuwa huduma anayoitoa anaweza
kuiboresha na kufikia watu wengne wengi zaidi ya wanafunzi wa pale chuoni. Leo
hii ni historia.
ü Tabia ya kujenga mahusiano. Unapo
deal na mteja mpya usikimbilie kumuuzia
tu huduma au bidhaa yako. Hakikisha unatengeneza mahusiano naye mazuri. Sio
swala la kuuza tu, unatakiwa kumfanya mteja awe na hamasa ya kurudi tena na
tena
ü Sikiliza, jifunze, Ongoza (Listen, learn, and lead). Ukisikiliza
kutakufanya ujue nini tatizo la
mteja wako. Ukijifunza unajiongezea maarifa unakua mwerevu zaidi hivyo kua na
uwezo wa kuongoza wateja kule unakotaka waelekee.
ü Kuandika maelezo (taking Notes) wakati
unapokutana na mteja mtarajiwa
(prospect) ni nyenzo ya mazuzo yenye nguvu sana(powerful sales tool). Hakikisha
wakati wa mazungumzo unaandika mahali ili kukusaidi kujua vizuri tatizo la mteja
wako mtarajiwa. Kuchukua maelezo pia kutakusaidia yafuatayo:
v Kuandika
kutakusaidia kusikiliza kwa makini, na itakua ngumu kusahau pointi muhimu
v Kuchukua
maelezo kunakuweka katika hali ya kua na mamlaka na uthibiti
v Kutaimarisha
uwezo wako wa uchambuzi. Maana unahusisha milango mitatu ya fahamau amabyo ni
Kugusa( unapoandika), kusikia ( unaandika ulichokisikiliza kutoka kwa mteja
wako), kuona (Unaona ulichokiandika)
v Kutakusaidia
kupata taarifa zaidi kutoka kwa mteja wako mtarajiwa. Maana atajisikia vizuri
kufunguka maana anaona unajali anchoongea na upo serious katika kutatua
changamoto aliyonayo
ü Tengeneza mpango wa kila mteja wako mtarajiwa.
Mpango utakua pia unaonyesha jinsi
gani ya kutatua tatizo lake kutokana na maelezo uliyokua ukiyaandika kwenye
vikao vya nyuma kama ilivyoelezwa kwenye pointi ya hapo juu. Mpango utakua ni
dira ya kufahamu ni kitu gani cha tofauti hasa unachoweza kufanya kwa huyo
mteja wako. Kusikiliza ndio siri ya kwanza, na kutambua suluhisho
zitakozokubaliwa na pande zote mbili ni siri ya pili.
ü Unatakiwa uwe daktari. Mfano: Unapokwenda hospitali labda
tumbo linakuuma kisasawasawa ,
Unapofika kwa daktari hautojali kwamba amehudumia wagonjwa wangapi au wagonjwa
wangapi wako wanamsubiri. Utakachopenda ni akuhudumie. Utataka akupeleke
kwenye
chumba cha matibabu kwa ajli ya uchunguzi na kukupatia matibabu sahihi kabla
hajakimbia kwenda kuhangaikia wagonjwa wengine. Utataka akuulize unajisiakiaje,
umekua na hali hii kwa muda gani, je ulishawahi kupatwa na tatizo kama hili
nyakati zilizopita, nk. Kama daktari akikufanyia hayo yote na akakupa matibabu
utafurahi na utakua na mtazamo mzuri zaidi kwake, na hata utapenda kuja kumuona
wakati mwingne. Pia utapenda kuwashauri wengne wenye tatizo kama lako waende
kwa daktari huyo kwa sababu ya huduma yake nzuri.
Hivyohivyo
basi mtu wa mauzo (Salesperson) au muuzaji ni daktari. Haijalishi umehudumia
wagonjwa (wateja) wangapi. Huyu mteja mtarajiwa (new propect/customer) ndio
yeye tu ambaye unapaswa kumuona kwa wakati huo, na kumhudumia kipekee.
Usimhudumie kwa harakaraka ili ukimbilie wengine, hakikisha umetatua tatizo
lake na ameridhika. Mfanye ajione yeye ni wa pekee kwa wakati huo unaomhudumia.
Kufanya hivyo hakuta fanya tu mazingira ya kaz yawe mazuri, bali pia kutaongeza
kupendwa kwako na wateja na kupelekea watamani kurudi tena na tena.
ü Onyesha kua na shauku. Unapohudumia wateja wako, au
unapokutana na mteja mtarajiwa
onyesha shauku. Hii itamfanya asijiskike kwamba ni wa kawaida tu, atajisikia
vizuri maana anona uko excited kukutana naye.
ü Jipe sifa unazo stahili. Ongea kuhusu wewe lakini katika hali
ya unyenyekevu ili islitete tafsiri
ya kua unajivuna. Uongee kwa ujasiri kuhusu biashara yako na mambo amabayo
inaweza kutatua, cha muhimu epuka mbwembwe nyingi zisizokua na maana.
ü Jifunze kusoma hali na nyakati. Sio
kila kinachofaa kwa mteja A kitafanya kazi
kwa mteja B… You have to learn how to read the situation
ü Kuwa
mtalaamu. Kwa
wataalamu wengi wapo makundi mawili;
v ·Kundi
la kwanza ni lile la wataalumu ambao wanaongeza thamani kwenye kila kitu
wanchokigusa au kukifanya.
v Kundi
la pili ni wale wanaofanya thamani ya kila wanachoguza ishuke.
Kama
wewe ni mtaalamu thibitisha kwamba upo kwenye kundi la kwanza. Onyesha thamani
yako. Hakikisha kila unachofanya unaongeza thamani yake.
ü Ukweli ni nyenzo muhimu. Unapaswa kua mkweli maana ndio rahisi kuukumbuka. Ukweli ni rahisi
kuukumbuka kuliko uongo. Ndo maana wanasema ukiwa muongo uwe na kumbukumbu
vizuri, maana utaumbuka tu siku moja. Hakikisha unajenga uaminifu na wateja
wako kwa kua
mkweli. Tell the truth; it‟s easier to remember. Don‟t promise your customer
what you can‟t deliver.
ü Jiuze kwako mwenyewe (Sell Yourself on Yourself).
Jihamasishe mwenyewe kwanza kabla ya
kuhamasisha wengine. Kabla hujajiuza kwa wengine anza kujiuza kwako kwanza.
Taswira yako mwenyewe (Your self-image) ni ya muhimu sana. Utakavyojiona ndivyo
na wengine watakavyokuona.
ü Mhusishe mteja. Usiwe wewe ndo muongeaji tu mwanzo
mwisho. Mfanye aongee kuhusu yeye
mwenyewe. Hii itafanya akupe taarifa ambazo utajua ni suluhisho gani anahitaji.
Hata kama unaongea usijisahau ukaongea tu kuhusu wewe na biashara yako.
Hakikisha kunakua kwa faida yake. Mpe nafasi pia atoe maoni yake.
ü Anza mapema siku yako. Hii ni moja ya siri za watu
waliofanikiwa. Unapoanza mapema
unashauriwa kupata wasaa wa kutulia pekee yako na kutafakari. Wakati huu ni wa
kwako na wewe, unahojiana na wewe mwenyewe. Unaichaji akili yako na utaona
utofauti. Ukichunguza watu wanoamka alfjiri na mapema na wale wanoamka sa 2
asubuhi utendaji wao wa kazi ni tofauti sana. Kwa watu wengi alfajiri ndio
wakati akili inakua na nguvu. Mimi mweneywe siku nikiamka mapema afajiri hua
nakua na hamasa kubwa ya kazi. Lakini siku umechelewa kuamka, kwanza unakua
huna raha, unaona umechelewa, unakosa muda wa kutafakari au kumuomba Mungu, na
hata ukitafakari wakati umeamka kwa kuchelewa akili yako haitakua imetulia
maana muda wote inawaza saa ngapi utafika kazini. Ukijijengea tabia hii ya
kuamka mapema na kuutumia muda huo kufanya vitu vya maana lazima utaongoza
kwenye sehemu uliyopo, iwe biashara, kazini n.k
ü Usisikilize redio au kuangalia TV asubuhi. Habari
nyingi utakazosikia au kuziona
wakati huo ni habari mbaya (hasi) amabazo zitakutia hofu na
kukukatisha
tamaa. Badala yake tafuta CD au video au chochote kile cha kuhamasisha. Hakikisha
siku yako unaianza kwa hamasa kubwa.
ü Soma vitabu, majarida au machapisho yanayohusiana na
biashara au kazi unayofanya. Hii
ndiyo njia ya uhakika ya kukuweka juu, Maana utakua na maarifa makubwa ambapo
yatakusaidia katika ubunifu. Ukisoma ukafikisha vitabu au machapisho 500 utakua
kati ya watu 1% ya wale waliofanikiwa sana katika hiyo biashara au kazi. Pia
hii itakuongezea kujiamini maana utakua umebobea na utakua mtaalamu wa
kutegemewa maana unataarifa nyingi zenye thamani kubwa.
ü Mteja sio mara zote yuko sahihi. “Mteja mara zote yuko
sahihi “ Hii ni moja kati ya
amri kumi za mauzo, na amri hii ya kwamba mteja yuko sahihi imekua ikivuka
kizazi hadi kizazi. Lakini si kweli kwamba mteja yuko sahihi mara zote. Lakini
haimaanishi kwamba umwambie mteja wako kwamba hayuko sahihi. Kua mbunifu katika
kuonyesha usahihi, aidha kwa kutoa kama pendekezo. Forget the conventional wisdom.
I t‟s okay to tell a customer that there‟s a better way.
ü Makosa hua yanatokea. Unapokosea haipaswi kujuuta mpaka unaharibu mambo mengine. Kua muwazi
kukiri kosa omba msamaha na kusonga mbele. Jifunze kutokana na kosa fanya
maboresho husika.
ü Ona fahari ya kile unachokifanya au unachouza. Mwambie kila unyekutana naye kuhusu kampuni unayofanya kazi na bidhaa au huduma zinazopatikana.
JISAJILI KOZI YA KUONGEZA MAUZO MENGI