Watu
wote ambao hatuna mitaji, hela na wala hatukui kibiashara ni kwasababu moja kuu
hatuna mtandao wa watu wenye hela.
Ukifungua simu yako,utakutana na namba za watu wa aina gani?
Wana hela?
Kabla
sijasema neno hapa ngoja kwanza nikupeleke kwenye familia za matajiri duniani.
Familia kama Rockerfeller Family, Rothschild family…na nyingine duniani
utakutana na tabia ambazo zimeridhishwa vizazi na vizazi. Ukikutana na familia
masikini duniani utakutana na vijitabia vimerithishwa vizazi na vizazi….kutoka
kwa babu, baba, mtoto na wajukuu na vitukuu huko.
Tukianza
na hii familia ya Rockerfeller inafahamika duniani kibiashara. Ni familia ya
kibiashara. Tukimfuatilia mjukuu David Rockerfeller alipokufa miaka ya hivi
karibuni alikufa akiwa billionea na Zaidi alifahamika kama guru wa kukusanya
mtandao wa watu wenye thamani ya mabilionea. Siri kubwa ya familia za kitajiri
ni kuwa na mitandao ya watu wenye thamani ya mabilioni.
Mfano
huyu David Rockerfeller alikuwa na zaidi ya namba mawasiliano za watu wakubwa
na muhimu kwenye biashara zake zaidi ya 200,000. Yaani ni hivi alikuwa na
business cards za watu muhimu duniani hasa wenye hela. Utaniuliza alizitunza
wapi?
Kuna
hii kitu inaitwa Rolodex ; ni kama file Fulani la kutunza kadi. Yaani huyu
David huyu alikuwa na Rolodex yenye urefu wa futi 5 imetunza kadi za watu
muhimu kwenye biashara zake; jaribu kufikiria wewe hapo una kadi ngapi or namba
za watu muhimu wangapi wenye hela?
Kitu
cha ajabu, ngoja nikuambie namna alivyokuwa anatunza kumbukumbu za hao watu
muhimu kwenye biashara zake..yaani watu wenye hela… Kwenye kila kadi inaonyesha
jina la huyo mtu, sekta gani yupo, biashara yake, muda mwingine hata utajiri
wake, taarifa zake zikionyesha alioa lini, kama aliachana na mke or mume wake lini
yaani alipeana talaka lini, mke wake ni nani, ana Watoto wangapi, mara ya
kwanza walionana wapi, namba za simu, email zake, nini waliongea kwa mara ya
mwisho…
Yaani
ni kwamba ukichukua Rolodex yake ina thamani ya matrilioni ya pesa. Nikikuuliza
Rolodex yako ina thamani ya shilingi ngapi? Au huna hata rolodex? Ukiona hadi
picha ya hiyo kadi , inaonyesha ameonana na Donald Trump mwaka 1971 , akatunza
kumbukumbu lini ameoa, lini alimtaliki mke wake sijui mwaka 90 na 93 akaoa tena
yaani taarifa zote muhimu.
Unadhani
Ray Croc aliweza vipi kupata wawekezaji kama si kwa kutumia mtandao wa watu
wenye pesa aliokusanya na kutunza?
Yeyote
yule ambaye ni Tajiri duniani, yeyote yule ambaye ni mwanasiasa mkubwa duniani
ana rolodex yake yenye thamani ya matrillioni na atakuambia kuwa hakuna thamani
kubwa duniani kibiashara kama thamani ya mtandao ulionao. Kama huna mtandao
wenye thamani nakuhakikishia hata uwe na ndoto ya kuwa billionea sahau hii
safari mpaka utakapoanza upya kuzalisha mtandao wenye thamani na kutengeneza
rolodex yako yenye thamani ya mabilioni.
Rolodex yako inatakiwa iwe na thamani ya watu muhimu
wafuatao;
a) Watu wanaoweza kuwa chanzo cha mitaji ya biashara yako. Wewe unayelalamika kuwa sina mtaji si
kwamba huna mtaji ila ni kwamba huna watu wa maana. Huna watu ambao unaweza
kuwashirikisha na kuwashawishi kuhusu faida ya wao kuwekeza kwao. Hii haitokei
kiajari ajari lazima uwakusanye hao watu ndani ya rolodex yako.
b) Watu ambao wanaweza kuwa wanasheria wako.
Wanaoweza kukusaidia pale
unapohitaji msaada. Kuna dada mmoja alikuwa anataka muhuri tu wa mwanasheria
kwenye biashara yake, akaenda kwa wanasheria wakamwambia laki mbili. Nikampa
mawasiliano ya mwanasheria wangu akaenda kumpigia mhuri kwa Tshs elfu 10
kwasababu tu tunafahamiana na ni sehemu ya Rolodex yangu. Ni kama ndugu yangu.
Wanasheria wanaoweza kukusaidia kwenye biashara, pale unapokutana na ishu
muhimu
iwe kwenye real estate, umiliki wa kampuni, kodi na mengine mengi….
c) Mtandao mwingine ni watu wanaofahamika kama Connector; connector ni watu wanaomfahamu kila mtu muhimu.
Nina Rafiki yangu ambaye nikitaka namba ya mtu mkubwa Serikalini nitapata.
Yaani una kitu chako lakini unatafuta mtu ambaye anafahamiana na watu wa aina
mbalimbali basi ukiwa na connector Maisha yako yatapona.Hawa connectors
wanaweza hata kukuunganisha na wateja wakubwa wa biashara yako. Wana database
kubwaaaa ambayo ndiyo hii ya rolodex tunayoongelea.
d) Watu walio kwenye vyombo vya habari. Lazima
uwe na watu walio kwenye
media,kwenye TV, radio, magazeti na hata wenye influence kwenye social media.
Rolodex yako lazima ijaye watu wa aina hiyo.
e) Watu wenye taarifa muhimu kuhusu sekta yako, iwe
ni watafiti wanaojua sekta yako in
and out…wanaweza kuwa watalaamu nk.
f) Celebrities yaani watu maarufu, unatakiwa
kuwa na watu maarufu iwe kwenye
muziki, siasa, movie ..watu wenye sauti kubwa, watu ambao wanaweza kukupigia
kampeni na mambo yako yakaenda.
g) Wanasiasa. Hakikisha unafahamiana na wanasiasa,
viongozi wakubwa wa Serikali.
Kipindi cha nyuma wakati nina Chuo nilikuwa nawasiliana na Rais Kikwete na
nilifahamiana naye akiwa kama waziri wa Mambo ya ndani. Spika wa Bunge, yaani
walikuwa ndiyo watu muhimu walionipa hata sapoti ya kuniunganisha na Ruge
pamoja na Joseph Kussaga.
h) Watu wenye hela, watu wanaomiliki makampuni mbalimbali
ambao unaweza kuwauzia bidhaa or
huduma zako. Hapa ni database ya kufa mtu. Huwezi kuwa mjasiriamali au muuzaji
halafu huna database ya watu ambao wana sifa kubwa ya kununua bidhaa zako kwa
bei kubwa. Kama unauza sabuni basi hakikisha una wakurugenzi wa makampuni ya
usafi. Kama unauza chakula basi uwe na rolodex imejaa wamiliki wa hoteli , kama
unauza huduma nk…uwe na watu ambao hata ukiwaambia wakuunge mkono watakuja na
kukupandisha juu. Nakuuliza tena, Rolodex yako imejaa akina nani?
i) Watu
wenye mwonekano mzuri. Namaanisha watu
wenye sura nzuri.
Wanawake
wenye sura nzuri, wanaume wenye sura nzuri nk… Najua hapa utanielewa
vibaya…mimi sina tabia ya kuwa mnafiki hapa. Ukienda kwenye hoteli utakutana na
watu wenye mwonekano mzuri. Ukienda kwenye ndege utakutana na watu wenye
mwonekano mzuri. Watu hupenda kununua kwa watu wenye mwonekano mzuri.
Nilipoanzisha kampuni ya Global Corporate Performance tulikuwa na mdada mwenye
sura
nzuri sana simtaji jina lake akisoma ujumbe huu atanikumbuka. Huyu dada alikuwa
akienda kuongea na wateja lazima lazima wateja wampe cheque ….biashara ilikuwa
inaenda kwasababu ndogo unayoweza
kuidharau
mwonekano mzuri humfanya mteja kushawishika Zaidi…japo si kwamba ndiyo kila
kitu. Unaweza kuwaajiri or hata kuwatumia kwenye sherehe, or maonyesho nk…
10) Mwisho kabisa, mentors…, washauri wa biashara yako. Wanaoweza kukuongoza na kukuambia ukweli hapa
ulipofanya sipo. Hawa watu kitalaamu wanafahamika kama Sounding Boards. Hawa
watu wanaweza kukushauri or hata kukupa maelekezo n ahata kukuongoza…kumbuka
hawa mentors nao wana network kubwa wanaweza kuwa chanzo cha wewe kupata
network kubwa ya kuifanya rolodex yako iwe na thamani
Hawa
watu wote kwenye Rolodex wanaweza wasikusaidie chochote kama hutawafanya waone
umuhimu wako kwao. Narudia tena, hao watu wote hutanufaika nao kama hutawafanya
waone umuhimu wako kwao. Labda umekuja na namna ambayo unafanya biashara ambapo
na wao wananufaika kwa namna moja au nyingine, au labda mnasali pamoja na
mmejenga urafiki yaani kiimani na wanasimama na wewe kwasababu wanaona wewe ni
sehemu moja. Nilipokuwa nafanya kazi na Shigongo kama Rafiki yangu, tulikuwa
tunasali kanisa moja Word Alive. Waulize waliokuwa wanasali kanisa hilo Sinza
watakuambia wengi walidhani Shigongo ni ndugu yangu or kaka yangu.
Mfano
Haris Kapiga, kipindi anaanza kanisa lake nilikuwa kama muumini wake wa kwanza
…tulikuwa wachache na hiyo ikawa sababu ya mimi kufanya naye vipindi vingi
zamani kupitia temino ya clouds media ….kulikuwa bonding iliyokuwa
inatukutanisha…
Wengine
labda unaweza kujenga ukaribu kwasababu mnashabikia timu moja or mnaenda golf
pamoja or mnaenda kwenye mpira pamoja or mnakutana sana kwenye mpira pamoja or
kwenye maonyesho pamoja etc na unahakikisha mnafurahia pamoja…watu wa aina hii
watasimama kukusapoti kwasababu mpo pamoja. Hautapata shida kabisa kuwashawishi
au kuuza unachotaka kuuza kwao.
Wengine
labda mpo Chama kimoja. Mnapambana pamoja. Huwezi kuwa upo upinzani halafu mtu
unayetaka kuwa naye karibu ni waziri ambaye yupo CCM hamwezi kuchangamana, so
kibiashara lazima uchague moja …unataka kutumia siasa kunufaika kibiashara au
kudidimia kibiashara. Kwasababu hapa mtashirikiana pamoja kwenye chama,
mtafanya kazi pamoja za chama na hata ikiwa ni mambo ya kibiashara ni rahisi
mtu huyo kuwa msaada kwako. Wengine labda mnaweza kuwa ni mtandao wako na mkawa
karibu kwasababu mna adui wa aina moja yaani common enemy…
Mwingine
labda mmepitia changamoto pamoja, nakumbuka ukaribu tuliokuwa na Paul Mashauri
kuna changamoto tulipiitia pamoja. Kipindi nilipopoteza Chuo changu ni kipindi
alipopoteza kampuni zake za mwanzo ..so akawa ni mtu wa karibu kama familia
mpaka leo.
Mwingine
ni Rafiki wa Rafiki or Rafiki ambaye mnawasiliana naye. Nakuambia leo anza
kukusanya watu muhimu kwenye Maisha yako na kuwasogeza karibu. Anza kuwakusanya
iwe kuanzia kanisani, kwenye mikutano, misikitini nk…kusanya watu wa maana itakusaidia
kuwashawishi kuuza au kuwashawishi kwa chochote unachotamani kufanya.
Kuwa na
mawasiliano ya karibu na hao watu lakini usipende kuomba omba msaada kwao.
Jenga ukaribu ambao wao pia watakuona ni wa muhimu kwao. Angalia ni kitu gani
unaweza kuwafanyia nitakuambia katika sura inayofuata namna unaweza kuwafanya
wakuunge mkono kwenye chochote unachotaka wafanye kwaajili yako,
Jifunze
kutumia muda mwingi kuwa na watu wa muhimu kwenye Maisha yako, watu wenye hela
, matajiri. Watu wanaopambana kwenda juu.
Haiwezekani
ushinde na mtu asiye na hela eti kwasababu ni jirani yako or ndugu yako. Huwezi
kuwa na hela kwa kushinda na watu masikini hata kama ni ndugu zako or rafiki
zako or majirani zako.Hata ukinielewa vibaya potelea mbali. Siku nzima
mnaongelea visivyozalisha hela, unategemea nini?
Lazima
uwe karibu na watu wenye hela or watu muhimu niliowataja kwenye rolodex yako
ili ufikiri kihelahela, utende kama mwenye hela, utembee kama mwenye hela, uwe
ni mtu unayewaza au kufikiri kama wenye hela .. Kuliko kucheza mpira na vijana
wa mtaani kwangu bora nikalipie michezo ya golf hata kama sijui kucheza nikae
karibu na wenye hela nijenge undugu or urafiki na kubeba kadi zao za biashara.
Kama
huna watu hakuna biashara. Kama huna watu hakuna kanisa. Kama huna watu hakuna
misikiti. Kama huna watu hakuna vyama vya siasa. Ukiingia kwenye sanaa ya kuuza
ujue kwamba umeingia kwenye kazi ya kutengeneza mtandao na watu muhimu. Wewe
unayekesha unazalisha bidhaa wakati huna watu, kama bidhaa zako unazozalisha ni
sabuni utaoga mwenyewe na majirani wawili watatu na hutafika kokote…
Unapoenda
kanisani nenda kasali ukue kiroho lakini usisahau kuzalisha watu wa kujaza
kwenye rolodex yako.
Unapoenda
msikitini nenda kwaajili ya ibada na kiroho lakini usisahau kuzalisha watu wa
kujaza kwenye rolodex yako.
Unapoenda
mpirani usiende tu kushangilia simba na yanga, nenda kakutane na watu wa kujaza
kwenye rolodex yako,
Unapoenda
kwenye maonyesho usiende tu kuonyesha bidhaa bali nenda kakutane na watu muhimu
wa kujaza kwenye rolodex yako,
Unapoenda kwenye msiba usiende tu kuomboleza nenda kakutane na watu wa kujaza kwenye rolodex yako….Kuna Rafiki yangu nilimwambia aende
kwenye msiba badala yangu, msiba wa Mengi…na nikamsihi sana nenda ukaomboleze lakini usisahau kukusanya watu wa kujaza kwenye rolodex yako, nilipoenda kwenye msiba wa Ali Mufuruki nilienda kumuomboleza mentor na mwalimu wangu lakini pia nilienda na kukusanya watu wa kujaza kwenye rolodex yangu.