Loading ...

0
Fursa 101 Africa Academy . 13th Jun, 2021

Unaelewa Business Model yako?

MTINDO wa Biashara (Business model)
“M” ya pili katika “M” sita ni MTINDO WA BIASHARA YAKO – BUSINESS MODEL.
KAMA HUJUI UTAINGIZAJE HELA KWENYE BIASHARA UNAPOTEZA MUDA. NA WALA USIHANGAIKE KUMTAFUTA MWEKEZAJI. HAKUNA ATAKAYEHANGAIKA NA WEWE.
Swali la kujiuliza kuhusu mtindo wako wa biashara ni hili: Biashara yako itaendeshwaje na utapataje hela?
Kama una wazo la biashara kubwa kuliko facebook halafu ukiulizwa namna utakavyotengeneza hela unaanza kubabaika , huna maelezo ya kueleweka …achana na hilo liwazo likubwa unapoteza muda.
Kuna rafiki yangu mmoja alikuja, Tenganamba nina wazo la kutengeneza APP ya kuhesabu watu Tanzania. Alikuwa ameandika mpaka business plan page 50. Yaani wazo lake lilikuwa ni kubwa , namna alivyokuwa anaelezea mpaka anasikia raha.
Nikamuuliza swali moja tu “Utatengenezaje hela?” Alibabaika sana akaishia kusema eti “Serikali itanilipa” Nikamwambia “Serikali hii tunayoijua ya Tanzania ikulipe hela…. Eeeh?”
Akasema watu watamlipa, nikamuuliza “watu watakulipaje?” Jaribu kufikiri mimi nimekuja mtaani kwako na wazo la kuhesabu watu na nikakuhesabu wewe mwenyewe utanilipa hela nikikuhesabu wewe?
Ilibidi arudi nyumbani kufikiri upya.
Unaweza kusahemewa kama wazo ulilonalo mwaka wa kwanza lisikuingizie hela by the way ni hatari kuliko maelezo, lakini miaka nenda rudi wazo halikuzalishii hela ni la nini hilo wazo.
Kama hujui vipi biashara yako itaingiza hela fahamu kuwa unapoteza muda. Hata makanisa siku hizi ambayo hayaingizi hela yanafungwa sembuse biashara…
Microsoft, mtindo wao wa biashara ni kutengeneza software halafu wanaingiza hela kupitia leseni,
McDonalds, mtindo wao wa biashara ni kutengeneza mtililiko wa menu ya Chakula na mfumo wa kisasa wa utendaji yaani operations kisha wanatengeneza hela kupitia franchising na real estates kwa wale franchisee. Unanifuatilia kweli?
NIKE, mtindo wao wa biashara ni kudezaini viatu kisha kutafuta wazalishaji wa viatu na kuuza kuuza kwa wateja wao na stores zao na kwa wasambazaji wao..
NETFLIX, mtindo wao wa biashara ni kuzalisha movies na kuingia mkataba na wazalishaji wa movies kisha wanaziingiza kwenye mtandao wao na kuziuza kwa subscription kila mwezi,
COCACOLA, mtindo wao wa biashara ni kutengeneza soda recipe yaani formula ya soda kisha na kuuza kwenye makampuni ya vinywaji duniani,
FACEBOOK , mtindo wao wa biashara ni kwamba wanatoa platform yao bure uitumie bure kisha ujaze data zako bure tena hulazimishwi halafu wao wanazitumia data zako kwa kuziuza na kufanya matangazo,
SOKOWORLD, mtindo wao wa biashara ni kuungana na wauza genge wote Tanzania, kuwapa mtililiko wa uuzaji (smart genge distribution model) kisha wanaungana na wakulima kuuza bidhaa kutoka shambani mpaka kwenye magenge na kupata hela kwenye kila mauzo. Sijaongelea e commerce hayo ni maandalizi tu ya awali.
Kama unaingia kwenye biashara na hujui mtindo wa biashara yako yaani business model utaingizaje hela unapoteza muda.



Shopping Cart

Loading...