Tufanye
kuna watu wawili. Mtu wa kwanza ana wazo kubwa sana linaloweza kuibadili dunia.
Labda wazo hilo linaweza kuwa sawa na Facebook au Uber ya sasa.Nikukumbushe
kuwa yapo mawazo makubwa zaidi ya facebook au uber, na kuna watanzania
nimekutana nao wenye mawazo makubwa mpaka unatetemeka lakini hawajui kuuza.
Mtu
wa pili yeye hana wazo la kutisha kiivyo. Kwa kifupi ni kuwa hana wazo kabisa
lakini mtu huyu yupo busy kujifunza sanaa ya kuuza kila siku. Akiamka asubuhi
yeye ni kujifunza sanaa ya kuuza tu. Kuuza kuuza kuuza…..
Wakati
mtu wa kwanza yeye anaamka na kuja na mawazo makubwa makubwa kama mtume
aliyeoteshwa.
Huyu mtu wa pili yeye anakesha usiku na mchana kujifunza
sanaa ya kuuza.
Nikiwa
mwekezaji kamwe sintaweka pesa zangu kwa mtu wa kwanza mwenye mawazo makubwa
makubwa. Nitawekeza pesa zangu kwa mtu anayekesha usiku na mchana kujifunza
sanaa ya kuuza.
Kwa
mfano, wa Ray Croc na hawa wakaka wawili Dick na Mac McDonald waliokuja na wazo
la McDonalds ungewekeza kwa nani?
Ngoja nikupe mifano ya watu maarufu unaowajua DUNIANI.
Mtu wa kwanza ni Mark Zukerberg unamjua? Najua unamjua….na
utasema
yeye
ndiye aliyekuja na wazo kubwaaa la Facebook. SI KWELI. Huu utafiti utakushtua
kidogo. Nifuatilie. Nitakuelezea. Facebook ilianza Desemba 2004. Unajua nani
alianzisha wazo la facebook? Wote tunamjua Mark Zuckeberg si ndiyo?
Sasa
leo ninakuambia ukweli aliyebuni wazo kubwa la facebook ni Mapacha wawili
waliojulikana na kama Winklevoss brothers. Walikuwa na wazo kubwaa la facebook
lakini Mark Zuckerberg akalichukua. Au Unaweza kusema aliiba, aliwapora,
vyovyote vile utakavyosema lakini yeye ndiye aliyesimamisha Facebook ikafahamika
hivi leo.
Mark
Zuckerberg akiwa ni mwanafunzi aliitwa na hawa wakaka Winklevoss Brothers
wakiwa wote ni wanafunzi kutoa mawazo yake kuhusu mfumo kama wa facebook ambao
tayari walikuwa wameshautengeneza kwa hatua za awali lakini haukuwa hewani .
Walitaka mawazo yake kwasababu Mark alikuwa
mzuri
sana kwenye coding yaani kutengeneza mfumo. Akausoma mfumo wote kwa umakini
halafu kesho yake akaanza kuutengeneza mfumo wao kama ulivyo. Akamshirikisha
rafiki yake Eduardo aweke hela ili mfumo uwekwe hewani.
, Eduardo
alitoa $18,000 mfumo ukaingia hewani. Mwanzo ilijulikana kama The
Facebook na ilikuwa kama
Harvard‟s yearbook. Fuatilia movie moja muhimu kuhusu facebook iitwayo, The Social
Network utanielewa.
Mfumo
ulipowekwa hewani , hawa vijana akina winklevoss brothers walishtuka kwasababu
wazo lao lilichukuliwa mchana kweupe, walienda kushtaki kwa mkuu wa chuo lakini
walichemka.
Zuckerberg
hakuishia hapo, alijua kabisa lile wazo linamhitaji mtu mmoja muhimu sana
kuliko kawaida ambaye ni muuzaji. Bahati nzuri muuzaji tayari alikuwa
ameshafuatilia kuhusu facebook ambaye ilikuwa inasambaa pale chuoni na kutumika
na wanafunzi karibu wote. Jina lake ni Sean Parker. Kama humjui Sean Parker,
huyu ndiye mwanzilishi wa Napster. Huyu jamaa ni muuzaji/sales guy. Mimi hupendelea
kuwaita watu kama hawa wauza maono.
Unaweza
ukawa na maono yako, wakayaona kisha wanahakikisha dunia nzima imeyajua maono
hayo, wakaleta hela, wakaleta wawekezaji wakaleta wateja… Ogopa
sana uwe na wazo kubwa halafu ukutane na muuza maono..umeliwa. Unamkumbuka Ray Croc?
Zuckerberg
akamwambia Parker nina wazo kubwa sana linaloweza kutuingia mamilioni ya
dollas. Parker akasema hapana hili siyo wazo la mamilioni, hili ni wazo la
mabilioni ya dolla.
Parker akaungana na
Zuckerberg …wakaingia kupiga kelele. Parker akafanikiwa kuuza maono ya facebook
kwa mwekezaji mmoja jina lake ni Peter Thiel, akawekeza dola 500,000 mpaka
facebook ilipofika level ilipo leo.
Dunia
nzima ikaijua Facebook ni kitu gani kwasababu iliingia katika mikono ya
muuzaji, Sean Parker.
Leo
hii Zuckerberg ana thamani ya $56 billion, wakati Sean Parker, muuzaji ana
thamani ya $2.6 billion. Haya sasa hawa akina Winklevoss brothers waliokuja na
wazo kubwa la facebook wanamiliki nini?
Winklevoss
brothers waliishia kumpeleka Mark polisi kwa bahati ndipo walipofanikiwa kupata
fidia ndogo ambayo ni ya thamani ya $200 million tu wakati wenzao ambao si
waanzilishi wa hilo wazo wanamiliki mabilioni.
Wasingekuwa
na hela kabisa, kama mahakama isingeamua walipwe hicho kiasi.
Hivi
wewe unadhani kama Mark Zuckeberg asingelichukua wazo hilo, kungekuwa facebook
leo?
Kama Sean Parker muuzaji , asingeingia tungekuwa na Facebook?
Mfano
mwingine ni Martin Eberhard, unamjua huyu mtu? Hebu google uone. Huyu ndiye
aliyekuja na wazo la Tesla. Ndiyo mwanzilishi wa Tesla, lakini dunia nzima
inamfahamu tajiri mkubwa duniani Elon Musk, mimi huyu jamaa namuita
mwanamapinduzi akawa kama mwanzilishi wa Tesla. Elon Musk hakuanzisha Tesla,
alipogundua kuwa Tesla inaweza kuwa mapinduzi makubwa kiuchumi duniani, akachukua
hatua. Akanunua, akaingia sokoni na kuuza visheni ya Tesla. Leo hii ana zaidi
ya $20 billion wakati mwenye wazo hajulikani na hana utajiri wowote.
Kama
huuzi, utauzwa na hata wazo lako kubwa ulilonalo linabebwa. Sina maana
wewe uibe mawazo ya watu na kuuza maono hayo duniani. Pointi yangu ni kwamba,
ukubwa wa wazo si chochote kama hutaamua kuwa kama akina Ray Croc,Mark
Zuckeberg, Sean Parker, Elon Musk na wengine wengi. Kama hutaamua kuwa muuzaji
sahau mafanikio. Hata kama mawazo ni makubwa vipi. Jifunze kuuza. Jifunze kuuza
jifunze kuuza. Tutazama zaidi kuhusu kanuni kuu saba za kuuza.
Kuna wazalishaji wengi sana lakini kuna uhaba wa watu wanaoweza kuuza mawazo. Ukijifunza kuuza, kila mtu atakuhitaji. Acha tabia ya kutafuta mawazo makubwa zaidi ya Apple, snapchat au facebook, jenga msingi wako kwenye sanaa ya kuuza maono. Ukijifunza kuuza hutakosa hela hata kama huna wazo kubwa.