Loading ...

0
Category

Entrepreneurship

Reviews

5 (1 Rating)

Preview this course

Course Description

Nakukaribisha UjuziNet.co.tz  ndani ya Mentorship Box.

 

Kuna mambo makuu 6 nitakusaidia na kukuletea matokeo 100% kibiashara ukinitumia kupitia Mentorship Box. Mimi ni mtu ninayefanya kwa vitendo kupitia biashara zangu kuanzia Sekta ya Kilimo, Elimu, Afya, Burudani na Nishati Mbadala. Nikiwa kama mwekezaji mwenza katika kampuni hizo…Ninajua na nitakuongoza kwa yafuatayo ndani ya MentorshipBox…

 

TAFITI ZA KIBIASHARA, FURSA NA UWEKEZAJI

Kukupa tafiti za Fursa na biashara katika Mkoa husika, nchi nzima na hata Africa. Kuanzia market research, taarifa na hata watu muhimu wanaoweza kukupeleka mbele kwenye fursa husika. Uwekezaji, Masoko, Mauzo, Fedha nk… Ndiyo maana nasafiri kila mkoa, natembelea nchi mbalimbali za Afrika na kukusanya data.

 

NAMNA YA KUPATA MITAJI NA WAWEKEZAJI.

Hii ikiwa ni pamoja na documents zote za kutafutia mitaji kama proposals, pitch decks na documents nyingine na hata contacts za wawekezaji kadhaa ikiwa ni pamoja na kuona namna biashara yako inaweza kusimama ili iwekezeke.

 

KUKUWEZESHA KUUZA NA KUKUZA MAUZO.

Namna unavyoweza kuongeza mauzo kwenye biashara yako, namna unavyoweza kutawala soko lako na kukusanya wateja...nk

 

KUCHUKUA HATUA.

Kama ni muoga wa kuchukua hatua na kuanza kitu au biashara au project yoyote inayohusu biashara fulani au fursa yoyote

 

KUJENGA MIFUMO YA BIASHARA YAKO.

Hii inakuwezesha kusimamisha na kuendeleza biashara kubwa itakayoishi hata pale ambapo haupo Ikiwa ni pamoja na kukujengea mfumo mzuri kibiashara . Kupata partners sahihi kwenye biashara yako na hata mradi wako...na hata kwenye kampuni yako.

 

KUAJIRI WATU SAHIHI NA PARTNERS SAHIHI.

Kukuelekeza na kukuunganisha na watu sahihi au kujifunza namna unaweza kuajiri na kuwaongoza watu kwenye kampuni yako kubwa.

 

Ndiyo maana nakuhimiza sasa…ingia na jisajili ndani ya Mentorship Box (Anza, Jenga na Kuza Biashara  au Taasisi Yako)

 

 

Nakukaribisha sasa kwenye program ya Mentorship Box ya mwaka mzima. Mentorship hii ni kila siku ikiwa ni pamoja na maongezi ya simu moja kwa moja kwa kila mtu.

Programu hii ni tofauti na programu nyingine. Ni two way communication. Yaani kila aliye humu ndani lazima atoe ushirikiano wa moja kwa moja kwa vitendo kutokana na maelekezo atakayopewa.

Programu hii itakuwa na mambo yafuatayo:

 

a) Passive Mode

Hii ni session ya kwanza, inayokulazima mwanafunzi humu ndani kufuatilia kwa umakini masomo yatakayotolewa kwa maandishi, sauti na video. Kuna vitabu ambavyo kila mtu amepewa na kama hujapata hakikisha unavipata. Ndani ya mwezi mmoja, kila mtu humu ndani aliyenikubali kuwa mentor wangu kuna vitabu kuanzia 5 ambavyo ni lazima uvisome ndani ya mwezi huu mmoja kwani vimebeba hatima ya mwelekeo wetu. Vitabu hivi vitatolewa humu. Kuna vitabu vya mauzo, vitabu vya sekta uliyochagua. Ndani ya Mentorship Box kuna Library ya Vitabu vya Kila aina, sekta mbalimbali kuanzia Kilimo, Ufugaji, Usafiri, Uwekezaji, Bima, Mazingira…yaani sekta zote unazozijua…kila mmoja atakuwa na uchaguzi wa kitabu gani anahitaji na kuangalia Library kama kuna kitabu chake…Ikitokea hakuna hicho kitabu basi anaomba ili kitabu kiongezwe kwenye Library ya Mentorship Box…Vitabu vinavyohusu uwekezaji, vitabu vinavyohusu masoko kiundani, vitabu vinavyohusu uendeshaji wa biashara kuanzia kuanza mpaka kuendesha, vitabu hivi vitakutengeneza kuwa mtu sahihi. Kuna audio contents, kila mmoja analazimika kuzisikiliza kwa umakini, kuna video ambazo nyingine ni case studies za biashara mbalimbali unazoweza kujifunza kupitia wenzetu majirani wanavyofanya, wafanyabiashara nk…Hizi zote ni passive..yaani ni contents za kiundani haswaa. Hapa nakuomba sana ukae mkao wa kusoma …manake ni masomo ya nadharia zaidi. Hapa ni zaidi ya MBA ..Utakuwa bora kuzidi aliyemaliza MBA

 

Session hii itaambatana na kila mwanafunzi kumjua mwanafunzi mwenzake na kujiuliza mwenyewe ni kitu gani naweza kushirikiana naye, lazima ujiulize anauza nini na naweza kumuuzia nini, inawezekana unaweza kuwa mteja wake au akawa mteja wako kulingana na uhitaji, hivyo usiishie kusikiliza na kujifunza lazima ujifunze namna ya kushirikiana na wengine ambao kuna comments mbalimbali ndani ya Kozi utakutana na wenzako na kuchat na wenzako, biashara ni kushirikiana na watu, mjue kila mwanafunzi na kuona nini unaweza kumuuzia au kumsaidia, lazima kila mmoja ajifunze namna ya kutumia Golden Rule na kuunganisha nguvu pamoja. Natamani watu kutoka humu wawe ndugu, marafiki na familia zinazopendana na kuunganishana ikiwa ni pamoja na kusaidiana. Yapo mengi sana hapa endelea kufuatilia…

 

b) Practice Mode.

Katika session hii ni kwamba, tofauti na wengine wanavyofanya kwenye masomo yao, huwa wanaishia hatua ya kwanza. Mimi naenda zaidi. Hii ni mentorship ya tofauti. Kila mwanafunzi lazima azame kiundani kupitia hatua ya kwanza, kuhusu sekta yake, wengine tayari wana biashara zao…hivyo kila mtu lazima afanye kwa vitendo. Nitakuwa na muda wa kujua nani amefanya nini kulingana na biashara au fursa yake. Kuna watu ambao nitawaunganisha kwa wadau mbalimbali, labda ni partners Fulani ..ambao unatakiwa kuwasiliana nao au kuwaona…Kuna watu ambao hawajaanza biashara ..nitakuwa na muda wa kujua kama ameanza ama la…lazima kila mmoja afanye…lazima uchukue hatua…ufanye kwa vitendo kwa yale uliyojifunza. Tutakuwa na muda wa kusikiliza kila mtu, kujua nini kizuizi kinachomzuia kuanza au kufanya kisha kwa pamoja tunakiondoa…Kila mmoja lazima aingie kazini afanye. Kama ni kuuza lazima tusikie umeuza kiasi gani na kwanini umeshindwa kufikia target. Tutawekeana target, na kupeana repoti kila mmoja nini umefanya na wapi umekwama na tunasaidianaje. Hii si mentorship ya kukaa darasani na kusoma bila matendo. Ukisoma lazima ufanye , lazima uchukue hatua kwasababu kutakuwa na repoti kila siku, au kila wiki kuhakikisha kila mmoja anafanya. Hii ni session ngumu sana ambayo kwa wengine wasiochukua hatua tutasumbuana sana. Mentorship siyo mwalimu anakaa na kufundisha kisha anakaa pembeni ni pamoja na kurepoti wapi na wapi umeenda, nini umefanya, umekwama wapi na tunashauriana nini kifanyike…hapa ni kila mmoja ..hakuna atakayebaki. Inawezekana biashara yako imekwama mahali tutakaa pamoja na kushauriana kila mmoja. Kuhusu mitaji, kila mmoja lazima tuhakikishe anajua kuomba mitaji, na awe na business plan pamoja na pitch deck na kila mmoja atajifunza na kuanza kuomba kwa wawekezaji, kwahiyo ni kila siku ni madarasa

 

c) Active Mode. Hapa ni session ambayo tunaenda mbali zaidi ya Practice Mode. Hapa nataka kila mmoja baada ya mwezi awe na biashara ambayo ipo active. Ndani ya mwezi mmoja kila mwenye biashara awe na matokeo ya kuonyesha kuhusu biashara yake ambayo ipo active. Kipimo cha mentorship hii kitakuwa siku ya mwisho, kuona nani amesimama na yupo active kibiashara. Yaani lazima kila mtu awe na kitu cha kuonyesha. Kama unaingia katika mentorship hii huna biashara basi ndani ya miezi mitatu lazima uwe na biashara hata kama bado hujakamilisha usajili lazima uwe active kukamilisha usajili na uwe na kitu unachouza na upo active. Kama ni project lazima ianze, kama ni biashara lazima ianze, kama ni kuendeleza biashara yako lazima tujue umepiga hatua kiasi gani mpaka ulipofikia….Baada ya hapa yaani mwisho wa mwezi kumaliza session, kuna wale waliofanya vizuri ndani ya mwezi kibiashara nitawafanyia surprise, kama hana mtaji, ajiandae kwa surprise ya kuunganishwa na diaspora wa kufanana naye au kitu kingine kikubwa kitakachompeleka mbele ambako hakutarajia.

 

Kwa kumalizia naomba kila mmoja ajipange kufuatilia fursa zinazozalishwa na aina 10 za Trends zinazoendelea Afrika. Kuna trends zimejificha ambazo wengi bado hawajazijua zinazozalisha fursa mbalimbali kwa watu wajanja wanaoendana na mabadiliko yaani Trends. Naomba nianze kuzitaja

 

1. TRENDi YA MABADILIKO YA HALI YA HEWA YAANI CLIMATE CHANGE TRENDS. Wajasiriamali wengi kwa Afrika bado hawajaamka kuendana na trendi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Watanzania wengi bado hawajajua kwamba hata mitaji mingi ya pesa za bure inayotolewa na mataifa au makampuni ya kimataifa inapendelea zaidi wale wanaofanya biashara kwa kuangalia mabadiliko ya hali ya hewa. Mentor wangu mwenyewe aliniambia, Tenganamba angalia kama unaweza kuifanya biashara yako iendane na trends zinazoendelea duniani ili upate grants, yaani free money. Matunda yameshaanza kuonekana. Dunia inakokwenda si kule tulikotoka. Kuna viwanda vinavyozalisha hewa mbaya wanatafutwa wafanyabiashara wenye njia mbadala na mitaji ipo, kuna uchafuzi wa mazingira, wanatafutwa wafanyabiashara watakaokuja na majibu ya kufanya biashara zinazosafisha mazingira, yaani kuna mambo mengi sana ikiwa ni pamoja na fursa nyingi sana zinazozaliwa kupitia trend hii… Unafahamu kuhusu fursa ya kulima magugu bahari yaa sea weed? Unajua sea weed zinatumika kuzalisha bidhaa gani? Unajua Zanzibara kuna watu wametajirika kupitia Sea Weed? Unajua Bakhresa akiwa mdogo alianzia biashara ya kuuza vitu vya baharini ikiwa ni pamoja na sea weed ..hapo akiwa mdogo sana. Kuna vikombe vya plastic ambavyo degradable vinazalishwa na sea weed nitakuonyesha namna ya kufanya ndani ya mentorship lakini kwa wale ambao wapo au watapendelea fursa hii, nitakupa watu wa kuwasiliana nao na hata kuwatembelea au kuungana nao kwa Zanzibar na sehemu nyingine Tanzania.

 

Hivyo basi , trend hii imezalisha fursa kwa wajanja watakaokuja na BIASHARA YA KUZALISHA VIFUNGASHIO, BIASHARA YA INAYOGUSA MAZINGIRA ikiwa ni pamoja na kuzalisha bidhaa kupitia uchafu, green building materials yaani vifaa mbalimbali vya ujenzi vinavyozuia uchafuzi au uharibifu wa mazingira na nyingine nyingi nitakuelezea kwa wewe ambaye unazama kwa sekta hii nitakupa wapi uende na nani uwasiliane naye ili ufanye kwa vitendo.. Green transportation services or logistics etc, social enterprises ikiwa ni pamoja na tree planting…hizi ni fursa zinazopewa kipaumbele kwenye mitaji ile ya bure nitakuelezea ndani ya Mentorship Box…

 

2. TRENDI YA PILI NI AFROCENTRISM YAANI UAFRIKA.

Kumekuwa na trendi kubwa ya uafrika. Yaani kuna wateja wananunua vitu kwasababu ya uafrika, yaani vimebeba uzalendo wa kiafrika. Nitakupa mfano wa dada mmoja ambaye anatengeneza High end interior design yaani anazalisha interior design za kiafrika zinazouzwa kwa bei kubwa sana, anazalisha vifaa vya mambo vyenye uafrika na kuuza kwa bei kubwa, anazalisha fenicha za kiafrika, wengine wanazalisha milango ya kiafrika, wengine wanazalisha vitanda vya kiafrika, wengine wanajenga nyumba zenye mvuto wa kiafrika, wengine wanazalisha nguo zenye UAFRIKA, kuna wengine wanazalisha vifungashio vyenye mvuto wa kiafrika. Yaani nawajua mpaka wanafanya export ya Chai Iringa kwa mvuto wa KIAFRIKA.

Hapa kuna fursa za kufa mtu. Yaani ni balaa. Kwa wale watakaotaka kuzama hapa wataniambia lakini nitajua kulingana na mahitaji mtakayotuma inbox, nitajua huyu anatakiwa kujifunza nini na kufanya nini..

Trends nyingine kuanzia KULA KIAFYA NA LIFESTYLE yaani Health Eating and Lifestyle na nyingine saba tutazisoma ikiwa ni pamoja na Fursa zake zinazotokana na trends hizo na namna ya kufanya kwenye biashara yako kuendana na trends hizo tutashirikiana kwa ukaribu sana.

 

Gharama ya kuwa ndani ya MentorshipBox Tshs.750,000 kwa mwaka. Wengine hufanya mpaka Tshs.350,000 kwa mwezi na siyo mwaka.

 

Watu wafanyabiashara ambao nimewahi kuwafanyia Tshs.750,000 kwa mwaka.

Lakini sasa ninataka kukukaribisha rasmi kwa MentorshipBox ndani ya www.UjuziNet.co.tz . Kwasababu ni mgeni wangu rasmi naomba nikufanyie kitu ambacho sijawahi kufanya na sintafanya kamwe huko mbeleni… Ungana na wenzako kwenye MentorshipBox hii ambapo kama ukiamua kuingia sasa hivi  utalipia Tshs.55,000 tu na kupata Access ya Mentorship Box  mwaka mzima au zaidi. Gharama itakuwa inaongezeka kila mara mpaka kufikia Tshs.750,000 kwa mwaka lakini kama ukiamua kujiunga sasa hivi…hutakuja kulipia gharama yoyote itakayoongezeka. Maamuzi ambayo utafanya sasa hivi baada ya kuona tangazo hili yatakufanya uokoe Tshs. 695,000. Thamani ya MentorshipBox program na bei yake ya siku zote ni Tshs.750,000 kwa mwaka. Fanya maamuzi ya Kuchangamkia fursa hii kwa kuingia ndani ya Mentorship Box sasa hivi…kwa Tshs.55,000. Kuchelewa kwako kutakugharimu pesa nyingi …Fanya maamuzi sasa hivi…. Kwa Tshs.55,000. Ingia mara moja ndani ya www.UjuziNet.co.tz kama ukikwama kuingia kupitia mfumo wa UjuziNet nipigie simu au tuma meseji kwa whatsapp or kawaida kwa namba hii 0655973248. Ingia sasa ndani ya MentorshipBox..Ungana na wenzako waliojiunga kufanya makubwa..

 

 

 

Course Curriculum

1 Anza na Tabia Hizi kwanza
20
1. Vyanzo 15 Vya Mitaji Toleo 1
2. Sanaa ya Kuuza Toleo 1
3. Lima na Fuga Kibiashara Toleo 1
4. Sayansi ya Usindikaji Toleo 1
5. Africa is The Future Book 1
6. Become Creative Genius Book 1
7. The Richest Goldmine Within
8. Kichwa Chako ni Dhahabu Toleo 1
9. Kichwa Chako ni Dhahabu Toleo 3
10. Kichwa Chako ni Dhahabu Toleo 4
11. The Shift: Extra Ordinary Move
12. Mwongozo Kilimo Cha Tikiti, Mbegu,Magonjwa, Wadudu na Madawa
13. Kilimo cha Matango
14. Mwongozo Ufugaji wa Nguruwe
15. Ujenzi wa Bwawa La Samaki
16. Ufugaji wa Samaki Hatua kwa hatua Mwanzo Mwisho
17. Mifano Bora ya Mabwawa ya Samaki na Namna Bora ya Kujenga
18. Ufugaji wa Nyuki na Mwongozo wake
19. Ufugaji Bora wa Kondoo na Mbuzi
20. Mwongozo wa Ufugaji Bora wa Kuku wa Kienyeji
21. Kuandaa Mchwa wa Kulisha Kuku
22. Kanuni za Ufugaji Bora wa Kuku
23. Njia asili ya Kulea Vifaranga
24. Kitabu Cha Kutengeneza Vyakula Vya Kuku
25. Magonjwa Makuu ya Kuku na Tiba zake
26. Kutengeneza Mabanda bora ya Kuku
27. Njia Bora za Kulea Kuku
28. Mwongozo Uzalishaji wa Samaki
29. Uza kama Kichaa
30. Business Plan ya Restaurant ya Maua
31. Business Plan ya Mgahawa wa Kiafrika
32. Haulage and Logistics Business Plan

Student Feedback

Mentorship Box(Anza, Endeleza,Simamia na Kuza Biashara au Taasisi yako)

Course Rating
0.00%
0.00%
0.00%
0.00%
0.00%

No Review found

Sign In or Sign Up as student to post a review

Reviews

Shopping Cart

Loading...