Loading ...

0
Category

Entrepreneurship

Reviews

5 (1 Rating)

Preview this course

Course Description

JINSI YA KUBUNI BIASHARA KUBWA NA MIKAKATI YA KUANZA. (How to come up with Innovative Big Idea for Big Business)
KOZI HII NI BUREE KWA WATU WA MWANZO WATAKAOJIUNGA NA KUJISAJILI NDANI YA WWW. UJUZINET.CO.TZ 
JISAJILI KATIKA KOZI HII LEO BUREE. 
MAKAMPUNI MAKUBWA DUNIANI YALIANZA KWA KUBUNI WAZO ZURI.
WAZO ZURI NI KAMA MBEGU INAYO OTA, INAKUA NA KUWA MTI MREFU MKUBWA.
MAKAMPUNI MAKUBWA KUANZIA APPLE MPAKA GOOGLE.
EXXON MPAKA COCA COLA
ALIBABA MPAKA AMAZON
IPP MPAKA AZAM
EFM MPAKA CLOUDS MEDIA
MO ENTERPRISES MPAKA DANGOTE
MAKAMPUNI HAYA YOTE YALIANZA KAMA WAZO KUTOKA KWENYE KICHWA CHA MTU AMBACHO HATA WEWE UNACHO.
LAKINI LAZIMA UENDE ZAIDI YA WAZO ZURI KUJENGA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Lazima uwe na wazo zuri ili uwe na nafasi nzuri ya kufanikiwa kibiashara.
Njia rahisi ya kufeli kibiashara ni kuanza na wazo la ovyo.
Wazo baya linaweza kukugharimu muda na pesa.
Wazo baya linaweza kukuharibia mahusiano yako na watu ambao wamewekeza kwako.
Kila mwaka kuna watu wanaacha kazi na kuingia kwenye biashara na wazo la biashara baya. Na kupoteza kila kitu.
Kuna wastaafu ambao wengine wamewekeza pesa kwenye wazo baya la biashara, wakapoteza pensheni zao. Wazo linaweza likawa zuri kwenye akili yako lakini likawa baya kwenye soko lako.
Kuna watu ambao walifilisika kwasababu walianza na wazo baya.
Kama hutaki kupoteza pesa zako, kufilisika na kuishia kuwa masikini pamoja na kwamba una nia kubwa ya kufanikiwa kibiashara basi hakikisha unanifuatilia vizuri kwenye kozi hii.

Kama unatafuta wazo zuri la biashara ambayo ndiyo fursa yako,
Au kama tayari una wazo zuri la biashara utangulizi wa kozi hii utakufanya ujue kama upo njia sahihi.
Kabla sijaenda kukuonyesha namna ya kuja na wazo zuri la biashara, hebu kwanza tujue wazo zuri la biashara ni nini?
Wazo zuri la biashara ni lile wazo lenye sifa zifuatazo:

  1. Wazo zuri ni lile linalozalisha pesa. Kuwa na wazo kubwa ambalo hujui utaingizaje hela siyo biashara. Hata kama wazo lako ni passion yako, au hobby yako kama hakuna namna ya kuingiza hela hakuna wazo hapo. Wazo linaweza kuonekana kubwa. Wazo linaweza kukufanya ujisikie raha. Wazo linaweza kukufanya uonekane una akili sana lakini kama halitaingiza hela ni sawa sawa na bure. Halina maana. Wazo lako lazima likubaliane na soko, kwamba linaweza kuleta pesa. Wazo ambalo halikubaliki sokoni halina maana hata kama wewe unaliona ni kubwa.
  2. Wazo zuri ni lile ambalo linaendana na wewe. Yaani linaendana na mazingira uliyopo. Linakubalika na soko unalolenga. Linaweza kulipiwa na soko husika. Una ujuzi na vifaa vya kulitendea kazi. Una watu na koneksheni wa kukuwezesha au kulifanyia kazi. Kuwa na wazo kubwa bila ujuzi wa kulifanyia kazi , bila koneksheni ya watu wa kukusaidia kulitendea kazi ni ubabaishaji tu. Unahitaji watu wenye ujuzi ambao huna kusaidia wazo lako lifanye kazi, unahitaji watu wenye vitu ambavyo huna, unahitaji watu wenye pesa ambazo wewe huna ili wazo lako litembee bila hivyo wazo lako hata liwe zuri vipi ni sawa sawa na bure.
  3. Wazo zuri ni lile ambalo una uhakika nalo na unajiamini nalo. Kama wazo lako halikuhamasishi, halikusukumi kuchukua hatua kubwa na hata kutake risk basi hilo wazo ni ubabaishaji tu. Wazo la kujenga Microsoft , lilikuwa na nguvu kiasi ambacho lilimsukuma Billgate kuacha Chuo ili alifanyie kazi. Wewe wazo lako lina nguvu kiasi gani ndani yako? Wazo la kujenga Facebook lilimsukuma Marke Zuckerberg akadrop out kutoka shule. Wewe wazo lako likoje? Wazo langu la kuanzisha Smart Village Agri hubs limenifanya nihamie kijijini pamoja na kwamba nimeishi na kukulia maisha yangu yote mjini Dsm. Kuna watu wanarisk kufanya vitu kama vichaa kwasababu ya nguvu ya wazo linalowaendesha. Kama hujisikii nguvu na imani kubwa juu ya wazo lako , kama huwezi kurisk kupoteza chochote kwaajili ya kulifanyia kazi wazo lako maana yake wazo lako halina sifa na si la kwako.
Hivyo basi hizi ni sifa kuu za wazo zuri , ambalo ndiyo fursa yako. Fursa zote 101 utakazozipitia kama fursa hiyo haina hizo sifa tatu basi , siyo fursa yako wala siyo wazo zuri kwako.

WAZO ZURI LAZIMA LIINGIZE HELA.
WAZO ZURI LAZIMA LIENDANE NA WEWE.
WAZO ZURI NI LILE AMBALO UNA UHAKIKA NALO NA UNAJIAMINI NALO.
Katika kozi hii nitakuonyesha njia 11 za kuzalisha wazo zuri la biashara, na njia za kuyafanyia kazi. Hizi njia zinaitwa INJINI 11 za kubuni wazo zuri la biashara zilizosababisha kuzaliwa kwa fursa 101 na hata biashara kubwa kubwa unazozijua duniani.

Naomba kwanza nikuonyeshe safari kubwa ya wazo la biashara na njia ambazo lazima wazo hilo lipite:
  1. KUBUNI WAZO ZURI LA BIASHARA.Hapa ni pale ambapo, unakuja na wazo zuri, unaumiza kichwa na kubuni wazo zuri , hapa ni pale unapoanza kuwa na NDOTO. Watu wote tumepitia hapa. Hapa unaweza kuwa na mawazo mengi sana lakini lazima uingie hatua ya pili.
  2. CHAGUA WAZO LAKO BORA.Hapa ni kuchagua wazo bora linalokugusa lakini linalogusa zaidi soko lako. Linakubalika na soko lako.
  3. UHAKIKI WA WAZO LAKO KWA KITALAAMU IDEA VALIDATION.Hii ni hatua muhimu sana, ambapo lazima ufanye maamuzi ya kulihakiki wazo lako. Kivipi? Lazima utafute wateja wachache wa majaribio, wakikulipa pesa kwa wazo hilo basi hapo umeli validate. Kama hakuna mtu yeyote aliye tayari kukulipa pesa, wazo lako linahitaji kuangaliwa upya. Tutakuja kusoma kiundani kuhusu hilo mbeleni kwenye kozi hii. Kumbuka kwamba , kabla hujaingia na kuanza rasmi biashara kulingana na wazo lako lazima ulihakiki wazo lako kwa watu wachache wa karibu uone , ili usipoteze pesa nyingi kama ikitokea kwamba wazo lako halikubaliki na soko
  4. ANZA. Hapa ni pale ambapo unaingia rasmi kwenye biashara, baada ya kuhakiki wazo lako kwa wateja wachache sasa unaingia kwa kuwafuata wateja wengine wengi kulingana na kianzio chako. Hapa ni muhimu sana ukumbuke, wazo lililo kichwani halina maana kama hujachukua hatua yoyote. Ili uweze kubuni na kuja na wazo zuri la biashara lazima ujiulize watu wanapata usumbufu gani ?
    Unawezaje kuondoa usumbufu huo au kurahisisha maisha yao au kupunguza gharama au kuokoa muda wao au kutatua matatizo yao kama magonjwa au maumivu?
    Mfano, umewahi kujiuliza kwanini watu wanapendelea kutumia UBER na siyo Taxi za kawaida?
    Ule usumbufu wa mimi kutembea mpaka barabarani kutafuta Taxi za kawaida, Usumbufu wa kumsubiri dereva wa Taxi muda mrefu barabarani na anaweza asifike na asijali kabisa.
    Natumia UBER kwasababu inanipunguzia muda wa kusubiri, kuniondolea usumbufu na kunirahisishia.
    Soma sekta unayotaka, fuatilia muda unaotumika mpaka mteja kupata huduma au bidhaa, fuatilia usumbufu anaokumbana nao halafu angalia namna ya kuja na njia rahisi ya kuondoa usumbufu na kumrahisishia.

    Tuanze na hivi, Chagua sekta unayotaka halafu fuata hatua zifuatazo:
    1. MOJA,Soma mfumo mzima wa huduma wa sekta hiyo.
     Soma mfumo mzima wa kununua bidhaa mbalimbali za matumizi ya kawaida.
     Soma mfumo mzima wa kununua au kumiliki nyumba.
     Soma mfumo mzima wa kupata huduma za hospitali na hata kuonana na daktari.
     Soma mfumo mzima wa kuandaa chakula
     Soma mfumo mzima wa kujenga nyumba mpaka kuhamia
     Soma mfumo mzima wa kupata mke au mume wa maisha yako.
     Soma mfumo mzima wa kilimo mpaka bidhaa inamfikia mteja.
     Soma mfumo mzima wa kupata nyumba ya kupanga au ofisi

    2. MBILI, orodhesha hatua au stepu zote za mfumo wa huduma.
    Yaani hapa namaanisha, orodhesha hatua zote ambazo mteja lazima azipitie ili aweze kupata huduma au bidhaa anayotaka. Zipo hatua ngapi?
    Kwa mfano, nikitaka kununua bidhaa za wakulima kwa jumla nitapitia hatua ngapi mpaka nipate bidhaa hizo? Lazima niende sokoni asubuhi na mapema kuanzia saa 11 asubuhi au kabla ya hapo. Nitakutana na madalali wa sokoni wenye maneno mengi. Ikishindikana hapo, lazima nisafiri vijijini kwa wakulima, muda mwingine lazima nitafute sehemu ya kulala, lazima nione bidhaa zipo kwenye ubora mwenyewe, lazima nimlipe mkulima atakayeniuzia mazao hayo, lazima nitafute usafiri wa kusafirisha mazao yangu na hatua nyingine nyingi ambazo sijataja. Yaani ni usumbufu na kero za kutosha. Sekta nyingi Afrika zipo hivyo.

    3. TATU; Njoo na njia ya kupunguza hatua au stepu za mfumo wa huduma.
    Baada ya kujua mfumo mzima na hatua ambazo mteja lazima azipitie ili aweze kuhudumiwa, njoo na ubunifu au njia ya kupunguza baadhi ya hatua hizo. Hii ipo hata kwenye taasisi kubwa kubwa kama hospitali na mashule au hata taasisi za Serikali. Unajua nini, kampuni ikiwa kubwa huwa inakuwa na mambo mengi, sheria nyingi zinazohitaji kujaza sehemu nyingi. Inachukua muda mrefu na hatua nyingi sana mpaka mteja kupata huduma au bidhaa. Vipi je kama ukija na majibu ya kupunguza hatua zinazopoteza muda? Wateja wangapi watafurahia huduma yako?
    Sekta karibu zote zinahitaji mapinduzi haya. Utagundua kwamba zina hatua nyingi sana mpaka mteja apate huduma au bidhaa ambazo hazina maana na ni usumbufu kwa wateja. Je unaweza kuja na majibu ya kupunguza hatua hizo na kuhudumia wateja kwa urahisi?

    4. NNE, Fanya majaribio kwa wateja wachache waone namna ambavyo umepunguza hatua zisizo na umuhimu na onyesha namna ambavyo umerahisisha na kuondoa usumbufu.

    5. TANO, baada ya majaribio kwa wateja wachache, angalia wapi unaweza kuboresha au kurekebisha.

    6. SITA, ingia sokoni na kuanza kuuza huduma au bidhaa zako ambazo zimetokana na wewe kupunguza mlolongo wa hatua zisizo za lazima. Umerahisisha na kuondoa kero Fulani.

    Sikiliza nikuambie ndugu yangu, sekta zote zina kero ambazo zinatokana na mlolongo wa hatua ambazo mteja lazima azipitie zisizo za lazima. Zinapoteza muda, zinagharimu maisha ya watu, zinakera na ni usumbufu kwa mteja, Ukija na majibu ya kupunguza hatua hizo, tayari umeondoa kero Fulani au usumbufu Fulani.
    Katika Sehemu ya Tatu , nitakupa mifano ya taasisi mbalimbali au biashara mbalimbali ambazo zimepitia hatua hizo kutatua kero, au usumbufu Fulani.

    INGIA KATIKA KOZI HII BUREEE LAKINI KWA MUDA FULANI. WALE WATAKAOFANIKIWA KUJISAJILI MWANZONI NA KUANZA KUSOMA NDIYO WATAKAOFAIDIA NA KUENDELEA KUSOMA KOZI HII BUREE . SIKU ZIJAZO KOZI HII ITAWEKWA BEI NA ITAUZWA KWA WALE WATAKAOCHELEWA KUJIUNGA NA KUJISAJILI NDANI YA UJUZINET.

    Ninao uhakika kwamba wabunifu wengi watazaliwa baada ya kujua hatua mbalimbali kwa mifano na kuondoa kero au usumbufu katika sekta Fulani.
    Jisajili na kuanza kusoma kozi hii buree

    Jisajili kwa kozi nyingine nyingi ndani ya UjuziNet na ambazo zinaingizwa na kuongezwa kila siku.


Course Curriculum

1 Fursa Kupitia Matatizo: TATUZI
Preview 14
2 Mwendelezo Fursa Kupitia Matatizo
Preview 18
1. Kichwa Chako ni Dhahabu
2. Kichwa Chako ni Dhahabu 2

Student Feedback

Vyanzo 12 vya Fursa Zinazotajirisha na Namna ya Kubuni biashara kubwa

Course Rating
0.00%
0.00%
0.00%
0.00%
0.00%

No Review found

Sign In or Sign Up as student to post a review

Reviews

Shopping Cart

Loading...