Loading ...

0
Fursa 101 Africa Academy . 13th Jun, 2021

Acha Umimi Ili Ufanikiwe

Watafiti wanasema, kama huna mafanikio sehemu uliyopo basi ujue wewe ni mchoyo. Najua ni ngumu kunielewa. Ma capitalist tunaamini binadamu selfish ni masikini. Mtu yeyote masikini, ujue ana asilimia Fulani ya uselfish.

Unajua kwanini nasema hivyo?


Jitathmini mwenyewe…watu wangapi wanapenda kukufuata wewe kokote unakokwenda? Ukiona hakuna mtu anayehangaika kukufuata wala kutamani kuwa karibu na wewe ujue una asilimia Fulani ya ubinafsi. Wewe si chanzo cha mafanikio yao. Wewe si chanzo cha mazuri kwao. 


Je ni kweli huna kitu unachoweza kuwa mchango kwa wengine?


Waswahili wanasema Fuata nyuki ule asali. Ukiona hakuna anayekufuata ujue – hakuna asali.

Kuwa na tabia ya kutaka kupewa tu au kusaidiwa tu bila kujiuliza nini unaweza kutoa kwa wengine, ni tabia za kimasikini. 


Pointi yangu ni hii, ukitaka kufanikiwa kibiashara. Ukitaka watu wapende kuwekeza kwako. Ukitaka kila mtu atamani kushirikiana na wewe… basi uwe sababu ya asali. Hata kama huna hela, kama ni mtu unayesababisha mafanikio kwa wengine. Wanakuamini.


Billgate akifilisika leo…unadhani hatapata watu wengine watakaowekeza kwake? Watakakuja wengi sana. Unajua kwanini? Hii ni kwasababu wanajua ukiwa na Billgate lazima …baadaye utapata pesa. Ni sawa na nyuki.

Sasa basi, ukitaka kufika mbali kimaisha basi jifunze ujuzi wa kuwa sababu ya mafanikio kwa wengine.


Unapopanga mipango yako, usijiangalie wewe peke yako na familia yako. Fikiria pia watu watakaoshirikiana na wewe. Watafaidika vipi. Watu hao wanaweza kuwa wawekezaji. Partners. Wafanyakazi. Wasaidizi. …na hata watu wenye mtaji.Usipokuwa na akili hiyo, sahau mafanikio.


Wengi hawafiki kokote kwasababu akianza biashara anajiwazia mwenyewe na kitumbo chake. Jambo la ajabu…watu wa aina hii hata anapotaka mtaji; anajiangalia yeye. Umimi.


 Mfano, mtu anakuja..kaka nina idea kubwa sana ya kuanzisha App lakini sina…hela. Nisaidie Millioni moja. Yaani ukinipa hiyo hela utakuwa umeniokoa.


Mtu wa aina hii akija kwangu kesho yake namzimia simu. 


Okay, mtu mwingine anakuja na kusema bro..nina wazo la kuanzisha App …na nimepiga hesabu kuwa ukiweka million moja nina uhakika hiyo App itakufanya upate zaidi ya million mbili.

Mimi hata nikibakia na million moja sina tatizo. Sasa unaonaje ukinipa million moja nikufanye upate pesa.


Hebu niambie wewe utampa nani hiyo million moja?


Soma zaidi kwa kozi bure kwa kujisajili


Shopping Cart

Loading...