Loading ...

0
Fursa 101 Africa Academy . 13th Jun, 2021

Unahitaji watu "You Need Allies My Friend"

MAHITAJI ya Lazima.
NANI YUPO NYUMA YAKO?
“YOU NEED ALLIES MY FRIEND”
“M” ya nne ni MAHITAJI gani ya lazima unayohitaji kuwa nayo kwa lazima ili biashara yako iende? Unamhitaji nani? Unahitaji nini?
Hapa duniani hata uwe nani huwezi kufika mbali mwenyewe. Kama una roho ya kibinafsi nakuambia leo achana na biashara. Hata kama una mtaji uliotafuta mwenyewe kwa jasho lako mwenyewe sahau kufanikiwa kibiashara kwa kujitegemea mwenyewe.
Unahitaji maarifa ya masoko kiundani, unahitaji ujuzi wa kitalaam yaani technical knowledge inayohusu sekta yako, unahitaji wanasheria , unahitaji mtandao wa mitaji, unahitaji muda, unahitaji njaa , unahitaji mtandao wa wateja, unahitaji mtaji na mambo mengine mengi ili uende mbele.
Swali la msingi la kujiuliza hapa tena naandika kwa herufi kubwa NANI NINAMJUA ILI NIWEZE KUPATA VITU HIVYO? NANI?
Unataka kuanzisha Clinic na umeishia darasa la saba, fahamu unamhitaji mtu aliyesomea udaktari kuwa mwanzilishi mwenza ili muanzishe CLINIC yenu.
Unataka kuanzisha biashara ya kuuza SOLAR yaani umeme wa jua, unamhitaji mwanzilishi mwenza ambaye ni mtalaamu wa umeme wa jua msimamishe kampuni.
Mimi nipo pia kwenye fursa ya Afya lakini si Daktari, kampuni ya mwanzo ambayo nilitaka twende pamoja nikiwa na ndoto kubwa ya kuja kumiliki pharmacy , hatukwenda pamoja akapatikana mwingine tena Daktari inaenda vizuri sana bila hata uwepo wangu akiwa yeye ndiyo CEO,
Zipo kampuni kama tatu ambazo nimeungana na watu wenye uwezo kitalaamu mimi nakuja na mtandao wangu na wao wanakuja na ujuzi wao…
Pointi yangu hapa ni kwamba hakuna kisichowezekana kama ukiamua kuungana na wengine wenye vitu ambavyo huna. Wengi tunakwama hapa kwasababu tuna roho ya ubinafsi. Huwezi kufika popote bila wengine usijidanganye…
Unachotakiwa kuwa nacho ili biashara yako iende ni kwa kuungana na wengine, kuwapa njaa, shauku, kuwapandikiza ndoto, maono na malengo. Kuwapa watu shauku na njaa ya kufanikiwa kisha unaungana nao mnafanya kitu kikubwa pamoja.
Huwezi kuja kufanikiwa kibiashara kama hujengi MTANDAO WA WATU wenye vitu, ujuzi na maarifa ambayo wewe huna. Huwezi huwezi…“YOU NEED ALLIES MY FRIEND”
Watu husema hivi , katika mafanikio ya mwanaume nyuma yake kuna mwanamke. Leo ngoja nikuambie ukweli katika mafanikio makubwa ya mtu yeyote nyuma yake kuna mtandao wa watu waliomfikisha.
Wewe unayepiga kelele kuwa nina ndoto za kufika juu halafu huna mtandao ulio nyuma yako, hapo unaimba taarab. There is no way utafika kokote.
Unahitaji ushauri wa watu, unahitaji ujuzi wa watu, unahitaji imani ya watu, unahitaji pesa za watu na unahitaji mawazo ya watu. Kama kuna kitu unachotakiwa kujifunza kama mjasiriamali ni namna ya kutengeneza mtandao wa watu walio na vitu ambavyo wewe huna.
Usione biashara ninazofanya , sina haja ya kuanza kujisifia eti nilifanya mwenyewe. Ninakuhakikishia nisingeweza bila watu wengi waliofanya mengi kwenye maisha yangu. Sikatai kuwa kuna walionikatia tamaa kipindi nimeanguka na kupoteza mwelekeo lakini nakuhakikishia kuna waliosimama na mimi mpaka leo nipo hapa.
Sina haja ya kujikweza na kujionyesha eti ninajifikisha mwenyewe kwa bidii yangu peke yangu, kuna watu wapo upande wangu. Kwanza mimi nina mapungufu na kasoro nyingi sana sijapata kuona. Kuna watu wananifanya nijione kuwa naweza kuendelea pamoja na mapungufu na kasoro zote.
Ninapomuona mtu asiyeona umuhimu wa kuwa na wengine huwa namuonea huruma sana. Haijalishi una mtaji mkubwa kiasi gani au umetoka wapi kifamilia vyovyote unahitaji msaada wa wengine.
Ni muhimu kuwa na ujuzi wa kuzalisha bidhaa Fulani, ni muhimu kuwa mwenye akili sana na mawazo makubwa , ni muhimu kujua soko lako kiundani Zaidi yaw engine lakini fahamu kuwa vyote hivyo bila mtandao wa watu sahihi havina maana. Hutafika kokote. Utauza vitu viwili vitatu na kupata hela ya kula lakini kamwe hufiki popote.
Marehemu JACK WELCH , mtu ninayemwamini sana katika biashara alisema “sahau MBA , JIFUNZE kutengeneza mtandao” kwa kitalaamu wanasema forget the MBA. Learn to network.
Kwa mfano unataka kumpigia simu mtu mkubwa anayeongoza katika sekta Fulani ya kibiashara Tanzania, utatumia muda gani kumpata? Mimi nikitaka kupata namba ya Mo Dewji , nusu saa ni nyingi. Wewe utatumia wiki ngapi?
Kwa mfano unataka kumpigia simu mwanasiasa mkubwa Tanzania , utapiga simu ngapi kumfikia? Nikitaka kupata namba hata ya Rais wa NCHI nitapata. Wewe utatumia muda gani?
Kwa mfano unahitaji mtaji wa kuongezea kwenye biashara yako , unafahamu nani wa kuwasiliana naye? Atapokea simu yako na kukusikiliza au atakupotezea?
Una bidhaa yako mpya, unataka kuuza kwa uwingi kwenye taasisi Fulani , una namba za watu unaoweza kuwaelezea na wakasababisha yakatokea.



Shopping Cart

Loading...